Fatma Karume awacharua TRA asema wanawapa kesi wateja wake, leo hii wanawatumia maua ya Valentine acheni vichekecho

Wakili wa kujitegemea Fatma Karume amehoji tangu lini kuna upendo baina ya wananchi na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Amesema mnawaweka watu ndani kwa kosa la utakatishaji fedha kwa kisingizo cha kutokulipa kodi.

“Embu acheni kuwachekesha watu wasiyenahamu ya kucheka,” aliandika Fatma.

Fatma aliandika ujumbe huo baada ya kuona makopakopa ambayo yanaashiria upendo kwa TRA ujumbe ambao ulikuwa unaenda kwa wateja ikiwa ni siku maalum ya Valentine.

Fatma aliandika ujumbe huo “Tangy lini kuna upendo baina ya wananchi na TRA? Mnatia watu ndani kwa Money Laundering eti kwa madai ya kutolipa kodi #freeerickkabendera si kapigwa ML? Hebu acheni kuchekesha watu wasiyena na hamu ya kucheka,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *