Fatma Karume ahoji kwa nini serikali inamsaka aliyetangaza kutibu ugonjwa wa Corona

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, ahoji ni kwa nini serikali wanamsaka aliyejitangaza kutibu ugonjwa wa virusi vya Corona.

“Wanamsaka nini sasa? Nilidhani serikali haisaki watu wanaotibu kwa kutumia amani za wenzao?,” aliandika Fatma.

Fatma aliandika ujumbe huo baada ya kuona taarifa ya Naibu Waziri wa Afya, Dk. Faustine Ndugulile, kueleza kuwa serikali imetuma wataalamu kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali vya tiba na kujitangaza kuwa anatoa huduma ya kutibu ugonjwa huo hatari.

“Kasema anaweza kutibu ugonjwa huo wa hatari ambao hata sasa mataifa bado wanahaha kusaka tiba,”. Alisema Ndugulile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *