504 Wakamatwa na Jeshi la polisi nchini Tanzania

Jeshi la polisi nchini linawashikilia watuhumiwa 504 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuua kwa kutumia mapanga, matukio ambayo yalitokea mikoa ya Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora

Mkuu wa operesheni maaulumu za jeshi la polisi nchini Mihayo Mskela amesema hayo wakati akitoa taarifa ya tathmini ya operesheni maalum ya kudhibiti matukio ya mauaji, kupiga ramli chonganishi na makosa mengine.

Mskela amesema operesheni hiyo ilianza februari 3, 2020 na imefanywa kwa siku 11.

Watuhumiwa waliokamatwa ni wa mauaji wakiwemo wa kata mapanga 44, watuhumiwa 75 wa ramli chonganishi, Watuhumiwa 170 wa kufanya uganga bila kibali, unyang’anyi wa kutumia silaha, kupatikana na nyara za serikali, wizi wa mifugo pamoja na watuhumiwa wa makosa mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *