Tisa wauawa kwa kukatwa mapanga

Watu tisa Mashariki mwa Jamhuri ya Congo wameuawa kwa kukatwa mapanga.

Tukio hilo lililoibua wasiwasi miongoni mwa watu limetokea katika kijiji cha Manzati jana Februari 12, 2020.

Kutoka na mauaji hayo wanakijiji zaidi ya 200 wamekimbilia katika Eringite kwa kuhofia kushambuliwa.

Dulu za kimataifa zinadai kuwa tangu Oktoba mwaka jana watu zaidi ya 40,000 wamekimbia makazi yao kutokana na hofu ya usalama.

Hata hivyo jeshi la ulinzi la nchi hiyo kwa kushirikiana na na lile la umoja wa Mataifa Monusco limeahidi kushughulikia hali hiyo na kukomesha mauji ya raia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *