Papa achomoa suala la Mapadri waliooa

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amekataa pendekezo la wanaume walioko kwenye ndoa kufanya kazi kama makasisi katika jimbo la Amazon.

Katika mkutano wa kanisa hilo uliofanyika Oktoba viongozi wa kanisa hilo walipendekeza wanaume waliopo kwenye ndoa waruhusiwe kuwa makasisi ili kukabiliana na upungufu wa watumishi.

Katika kile ambacho kimetafsiriwa kama majibu yake kwa mapendekezo hayo leo Papa amekataa watu wasio mkasisi kutoa sakaramenti muhimu za komonio na kuungamisha waumini.

Dulu za ndani zinadai kuwa kuondolewa kwa kanuni ya useja kwa makasisi wa jimbo la Amazoni kungewakasirisha wahafidhina ndani ya kanisa hilo ambao wanaamini Papa wa sasa anaendesha kanisa hilo kiliberali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *