Mahakama kuu yamkataa tena Rais

Kwa mara nyingine tena Mahakama kuu nchini Malawi imemkataa Rais Peter Mutharika baada ya kufutilia mbali rufaa yake.

Mutharika na Tume ya uchaguzi nchini humo walikata rufaa kuitaka mahakama hiyo kutaka kubatilisha maamuzi ya mahakama ya kikatiba yaliyofuta matokeo ya uchaguzi wa Mei 2019.
Februari 3, 2020 mahakama hiyo ilibatilisha uchaguzi mkuu uliokuwa umefanyika miezi 9 iliyopita.

Baada ya maamuzi hayo wananchi waliandamana kusherehekea uamuzi huo wa mahakama ambao ni Mchungu Mutharika na wafuasi wake.

Uchaguzi utarudiwa kutokana na matangazo ya Tume ya Uchaguzi hata na hivyo uamuzi huo wa mahakama umepongezwa na wengi ndani na nje ya nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *