Fatma Karume asema Makamu wa Rais anaongea kama mwanasiasa na sio dikteta

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amesema  Makamu wa Rais Samia Suluhu anaongea kama mwanasiasa na sio dikteta.

“Mwanasiasa anaelewa mtaji wake ni kura za wananchi kwa hiyo anajali wananchi,” aliandika Fatma

Fatma aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akieleza kuwa dikteta hajali wananchi atahakikisha atashinda uchaguzi kwa kuwaumiza wapinzani na kuiba kura “Hiyo ndio hulka ya dikteta,”.

Aliandika ujumbe huo baada ya kuona taarifa ya Suluhu akitoa maelekezo kuwa wasiwapunguze mitaji kwani wakiwasimamisha, mkifukuza watu kwa sasa hivi ” kila unayemfukuza ana ndugu marafiki watamuunga mkono kwa nini mtengeneze nongwa sasa hivi,” alihoji Samia Suluhu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *