Dondoo za leo; Adhabu zitakazowakabili Kinana, Makamba, Polepole awarushia kijembe, Miaka 10 inatosha!

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini.

Zinazotikisa ni pamoja na adhabu watakazokula Kinana, Makamba zawekwa wazi, Polepole awarushia kijembe na Jaji Warioba asema urais mwisho miaka 10.

Karibu;

MAKAMBA,KINANA GIZA NENE

Makatibu wakuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba jana Jumatatu Februari 10, 2020 wameitikia wito wa kamati ya maadili ya chama hicho tawala nchini Tanzania iliyowaita kwa ajili ya kuwahoji.

Jana mchana walifika katika ofisi ndogo za  chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam na kupokelewa na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula pamoja na katibu mkuu, Dk Bashiru Ally.

Kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili za CCM, Toleo la 2017 ni adhabu mbili zitawakabili wastaafu hao;

Soma zaidi>>>

POLEPOLE AWAPIGA VIJEMBE KINANA, MAKAMBA

Polepole amenukuliwa akiwatupia vijembe vinavyoonekana kuwalenga Makatibu Wakuu Wastaafu wa ccm baada ya kukacha mahojiano juzi huko Dodoma.

“Wakati Rais anamuagiza Waziri Mkuu kwenda kukagua makontena bandarini yupo kiongozi mkubwa wa Chama sasa ni mstaafu alikuwa ana makontena 700 Bandarini na hayajalipa Kodi, alivyoambiwa alipe kodi sasa ana korosho hivi moyoni kanuna vibaya mno” Polepole

Soma zaidi>>>

MIAKA 10 INATOSHA!

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema wanaotaka kuongezwa kwa muda wa Rais kukaa madarakani kinyume cha katiba wana maslahi yao binafsi.

Akihojiwa na kituo cha ITV katika kipindi cha Kunani kuhusiana na maoni ya baadhi ya viongozi kutaka Rais kuongezewa muda wa kukaa madarakani kinyume cha matakwa ya katiba iliyopo sasa.

Jaji Warioba alisema endapo akikaa kwa muda mrefu sana ni dalili za mtu kuanzisha ufalme wake kama ilivyo kwa marais wa Afrika akitoka madarakani anamuacha mtoto wake.

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo hebu tuliangalie japo kwa ufupi suala hili aliloleta Mdau kwenye mitandao ya kijamii ,Akihoji kwenye sekta ya kubembeleza ni ya nani kati ya Mwanamke na Mwanaume?

Mdau anasema kuna wimbi kubwa la wanadada kudai wanaume wa siku hizi hawajui kubembeleza wanawake lakini enzi za wazee wetu wanawake ndiyo walikuwa wanafundwa na kufundishwa namna ya kumbembeleza mume na kumlea vizuri

Miaka ya sasa kumekuja utandawazi na kazi hiyo wanataka watukabidhi sisi wanaume, haiwezekani kutafuta wewe kutwa nzima unahangaika halafu ukirudi una kazi nyingine ya kumbembeleza mkeo

Anasema Mwanaume sio mtu wa kubembeleza bali ni mtu wa kubembelezwa kwasababu anapitia magumu na kufanya kazi mbalimbali ili mkewe apate mahitaji

Maoni yako ni yapi juu ya Mdau?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *