Sumaye atoboa siri ya kuhama CCM

Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye leo Novemba 4 ameweka hadharini siri yake ya kuondoka Chama cha CCM kujiunga na Chadema uamzi alioufanya miaka minne iliypipta.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema alijiunga na na upande usiounda Serikali ili kuuimarisha na haliluwa jambo jepesi ikizingatia nafasi aliyokuwa nayo kutokana na kuandamwa na dola yeye binafasi pamoja na familia yake.
Itakumbukwa kuwa Sumaye alihamia upinzani Agosti 2015.
“Nimekuja upinzani kwa lengo la awali la kuimarisha upinzani wa dhati ili kuuimarisha na kuchukua dola, Mimi sikuja upinzani kuja ┬áChadema kutafuta vyeo, wakati nahamia upinzani tayari vyama vilikuwa vimepanga wagombea tayari.”
Pamoja na mambo hayo Sumaya ametangaza uamzi wa kujivua uanachama wa chama hicho huku Mratibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Casmiri Mabina ambaye aliambatana na sumaye katika mkutano huo akiwasilisha barua kwa chama chake kuomba kujiondoa katika hiyo kutokana na yaliyojiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *