Dondoo za leo: Afungwa kwa kutishia kumuua JPM, Lissu ataka Kabudi atumbuliwe, Dereva Taxi auwawa kikatili

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Ni siku  nyingine tulivu tunakukaribisha kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Jamaa kufungwa kwa kutishia kumuua Rais Magufuli, kunani? Lissu nae ataka Waziri Kabudi atumbuliwe, nini kimejiri? Na Dereva Taxi auwawa kikatili Arusha. Kujua kwa kina kuhusu yote hayo, endelea kubaki katika ukurasa huu na usome zaidi.

AFUNGWA KWA KUTISHIA KUMUUA RAIS MAGUFULI

 

MAHAKAMA ya Mwanzo ya Ipembe mjini Singida, imemhukumu mkazi wa mtaa wa Minga, Bahati Martin (39), kifungo cha miaka miwili jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kutamka maneno ya kwamba atamuua Rais John Magufuli.

Mshtakiwa anadaiwa kuropoka maneno hayo Novemba 26, mwaka huu, huku siku ya pili yake (Novemba 27) Rais Magufuli na msafara wake ukipita mkoani Singida kwa njia ya barabara kwenda Chato.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Yohana Zakaria, alitoa adhabu hiyo juzi baada ya kusema mahakama imetibitisha pasi na chembe ya shaka kwamba mtuhumiwa alitishia kwa maneno hayo, kosa ambalo ni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (9) sura ya 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Soma zaidi>>>

LISSU ATAKA WAZIRI KABUDI ATUMBULIWE

Image result for lissu

Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi, anapaswa kuwajibishwa kwa kutumbuliwa kabla hajaharibu heshima ya nchi kwa kitendo cha Tanzania kujitoa mahakama ya Afrika.

Alisema kitendo cha Tanzania kujitoa katika mahakama ya Afrika ni kukanyaga haki za wananchi.

Soma zaidi>>>

DEREVA TAXI AUWAWA KIKATILI ARUSHA

Related image

Dereva Tax kakutwa ameuawa ndani ya Gari lake akiwa amefungwa mikono yake kwa waya jijini Arusha.

Kaimu Kamanda wa  polisi Mkoa wa Arusha, Koka Moita amesema  dereva huyo kukutwa ameuawa ndani ya gari aina ya Toyota Colora lenye namba T183 BAZ, likiwa uelekeo wa kutoka mtaa wa Elikiroa kata ya Lemara.

Amemtaja marehemu huyo kuwa ni Lembris Mollel (23) Mkazi wa Tengeru Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Kumalizia dondoo zetu, tuangazie mtazamo wa baadhi ya wadada au wasichana juu ya wanaume kusaliti

Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha mrembo Nana, Video Vixen akisema ya kwamba kuna utofauti kati ya wanawake na wanaume, hawezi kumzuia mwanaume kusaliti,  na anamruhusu amsaliti.

Anasema anajua mwanaume hawezi kutosheka na yeye kwa hiyo ni bora amsaliti, akirudi wawe poa na atazidi kumpenda. Ameongeza kuwa, mwanaume sio wa kubanwa.

Unaonaje kuhusu mtazamo huo wa Mrembo Nana? Yuko sahihi, ni ruksa kwa wanaume kuendelee kusaliti. Tupe maoni yako mdau wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *