Sumaye kuongea na waandishi wa habari kesho, atagusia uchaguzi wa Chadema

Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye kesho anatarajia kuongea na waandishi habari kuhusu uchaguzi wa viongozi wakuu ndani ya Chadema.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi uliopo jengo la LAPF Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Kutokana na kupigwa chini katika nafasi ya uenyekiti wa Chama hicho kanda ya Pwani hivi sasa wafuatiliaji wa siasa hapa nchini wanahamu ya kusikia kutoka kwake.
Kuna hisia na duru ambazo bado hazijathibitishwa zinadai kuwa huenda kiongozi huyo akatangaza uamzi mgumu ambao huko nyuma amejiapiza kuwa hatothubutu.
Sumaye alipugwa chini wiki iliyopita akiaa ndiye mgombea pekee katika nafasi hiyo na tukio hilo alilitafsiri kuwa ni adhabu aliyopewa kutokana na nia yake ya kutaka uenyekiti wa chama hicho Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *