Uzao mdogo chanzo cha Saratani kwa Wanawake

Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk Julius Mwaiselage amesema kuzaa  idadi ndogo ya watoto ni chanzo cha ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake
Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa Dk Mwaiselage amesema aina hiyo ya saratani inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wagonjwa wengi huku waathirika wengi wakiwa wanawake mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema wanawake wengi wa Dar es Salaam wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kutokana na kuzaa watoto wachache tofauti na ilivyo kwa wanawake wa mikoani.
“Ukizaa watoto wengi wakanyonya kuna uwezekano wa kupunguza hivyo vichocheo, huku mjini wanawkae wako hatarini zaidi kwa sababu wanazaa watoto wachache,”
Hata hivyo Dk Mwaiselage amezitaja sababu nyingine za ugonjwa huo kuwa ni kutonyonyesha kwa muda unaostahili, matumizi ya pombe, unene uliopitiliza na kutofanya mazoezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *