Sakata la mfanyabiashara na TRA: Amesema kesi aliyobambikiziwa na TRA, Mahakama imeifuta mwaka huu

 

Mfanyabiashara Ramadhani  Ntunzwe, ambaye alitajwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa, kuwa ni miongoni waliosumbuliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushikilia mizigo yake kwa miaka mitatu, amesema kesi aliyobambikiziwa  imefutwa baada ya kukosekana ushahidi.

Akizungumza na Opera News, amesema kesi hiyo ambayo ilikuwa katika Mahakama ya Wilaya wa Ilala hakimu ameifuta Februari 19 mwaka huu baada ya kukosekana ushahidi.

Amesema alijua haki yake ataipata ndani ya mahakama maana mashtaka matatu aliyofunguliwa mwaka 2017 alibambikiziwa na TRA.

Katika kesi hiyo alisomewa mashtaka matatu la kutokutoa risiti katika mashine,  kuacha kubandika TIN namba na hakutoa ushirikiani.

Majaliwa alimtaja mfanyabiashara huyo katika mkutano wa wafanyabiashara kutoka katika wilaya zote za nchini uliofanyika wiki iliyopita ambapo Rais John Magufuli aliwaita ili wajadiliane mambo mbalimbali ikiwamo changamoto wanazokutana nazo.

Akizungumzia changamoto alizokutana nazo, Ntunzwe alisema alinunua mzigo huo kutoka nchini Afrika Kusuni na kuupitisha katika mpaka wa Tunduma mwaka 2016 na kushikiliwa na TRA hadi Marchi mwaka huu pamoja na kulifunga duka lake na kumsababishia upotevu wa mali zake.

Ntunzwe alisema kushikiliwa mzigo huo ni baada ya kugoma kutoa rushwa ya Sh milioni mbili kwa maofisa wa TRA.

Katika mkutano huo, Rais John Magufuli aliagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwakamate watumushi hao waliohusika katika kuomba rushwa.

Pia TRA imeagizwa kufanya tathimini ya hasara waliyomsababishia mfanyabiashara huyo na kulipa gharama hizo.

Takukuru jana iliwafikisha mahakamani watu watatu ambao ni mtumishi wa TRA na askari wawili kwa tuhuma za kumuomba rushwa mfanyabiashara huyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *