CHID BENZI AMWITA TID MNAFIKI,ASEMA ANAJIFANANISHA NA HARMONIZE WAKATI NI MZEE..

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Chid Benz amemwita msanii mwenzake Khalid Mohhamed aka Tid kuwa ni mnafiki kwani amekua akimsema vibaya kwenye media lakini wakikutana anajifanya kusahau alichosema.

Wasanii wote wawili walishawahi kutumbukia kwenye kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na walikua miongoni mwa wasanii majina yao kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuwa ni watumiaji na waathirika wa madawa hayo.

Akizungumza na kipindi cha Block 89 cha Wasafi FM Chid Benz amedai kuwa wakikutanaga club TID amekua akionyesha wako poa na kama hajamsema chochote kwenye media vile “anaongea tofauti kwenye kipindi lakini ukikutana nae Club anaanza Chid nambie ndugu yangu nimekumis sana

Pia ameeenda mbali na kudai kuwa umri wa TID umeenda sana na anajisaulisha umri wake kwa kunyoa kipara na panki¬† ili kujifananisha na msanii Harmonize wakati umri umekwenda “sasa wewe unajisahaulisha age yako unanyoa kipara na panki .. ufanane na Harmonize na kina Rich Mavoko wakati hufanani nao ,wewe ni mkongwe mzee”

 

Katika baadhi ya interviews alizozifanya msanii TID katika vyombo vya habari nchin amekua akimkashifu/utani msanii huyo juu ya uathirika wake kwenye madawa ya kulevya.

Cheki hapa the intrview hiyo aliyofanya Chid Benz, Wasafi Fm

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *