Kesho ni siku ambayo Waislamu hususan nchini Tanzania wanasherehekea Sikukuu ya Iddi. Hii ni siku ambayo huambatana sana na kuchinja wanyama mbalimbali ili kupata kitoweo kwaajili ya chakula maalum cha Sikukuu hiyo,
Wanyama kama vile ng’ombe, mbuzi, ngamia, kondoo basi ndiyo huwa siku yao ya kupigwa kisu ama kuchinjwa.
Inawezekana hili tukio si la leo lakini ni tukio linalofurahisha na hivyo, tumeona ni vyema pia tukakuchangamsha kwa kucheka au kutabasamu msomaji wetu.
Ng’ombe kasema hakuna cha Eid wala Maulidi…hachinjwi mtu kutengeneza ubwabwa…kwa Mustini… ebo! pic.twitter.com/kSaefpr7nI
— Dan Nkurlu (@RevKishoka) June 3, 2019